Greenpeace yachukizwa na makubaliano ya COP29
24 Novemba 2024Matangazo
Jasper Inventor, mkuu wa ujumbe wa shirika la Greenpeace kwenye mazungumzo ya COP29 amesema watu wamechoshwa na wamekata tamaa. Inventor amesema ahadi ya mataifa tajiri kutoa dola bilioni 300 kwa nchi masikini haitoshi kwa mahitaji yao. Na kuongeza kuwa shirika la Greenpeace na wengine wanasubiri mkutano ujao wa COP30, huko Brazil, kurekebisha makubaliano yaliofikiwa sasa.
Nchi zinazoendelea na wanaharakati wengi hawakuridhishwa na makubalano yaliofikiwa leo huko Baku.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi tajiri zitatoa ufadhili wa dola bilioni 300 kwa mwaka, katika kipindi cha miaka kumi, kwa nchi masikini ilikupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.