Hoteli iliyoshambuliwa na Al Shabaab yadhibitiwa Somalia
29 Novemba 2022Matangazo
Katika tukio hilo watu tisa waliuwawa kwenye jengo lililotekwa na Alshabaab karibu na makaazi ya rais,kwa mujibu wa polisi.
Milio ya risasi ilisikika kutoka nje ya hoteli hiyo wakati vikosi maalum vya usalama vilipokuwa vikipambana na wanamgambo hao zaidi ya saa 12 baada ya kuvamiwa hoteli hiyo.
Tukio hilo la hujuma limeonesha uwezo wanaoendelea kuwa nao Alshabab ambalo ni kundi linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa al Qaeda,wa kufanya mashambulizi yanayoweza kusababisha wakati mwingine mauaji ya watu wengi katika mji huo mkuu wa Somalia.
Hujuma za kundi hilo zimefanywa katika wakati ambapo serikali ya rais Hassan Sheikh Mohamud inaendelea na operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi hilo.
Chanzo: reuters